Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu wa agenda za malengo ya Milenia (MDG's) yanayotarajia kufikia tamati 2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake, Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA Academy.
No comments:
Post a Comment