Wakazi wa Kata mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wanatarajia kunufaika na mradi wa maji safi na salama ya kunywa ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
Mradi huo wa maji ya visima unatekelezwa kwenye Kata tisa ambazo ni Magomeni, Sinza, Manzese, Kinondoni na Kibamba, Msasani, Temboni, Mzimuni na Msumi.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa miradi hiyo katika Kata nne za Manzese, Sinza, Kinondoni Shamba na Magomeni, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda amesema Manispaa yake imejipanga vema kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya mwezi Disemba na kuwataka Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuisimamia ili ikamilike kwa muda uliopangwa.
“Wito wangu kwa Madiwani, Watendaji na Wenyeviti muhakikishe mnaisimamia kwa nguvu zenu zote miradi hii ikamilike ndani ya muda tuliokubaliana na wakandarasi ili wananchi waanze kunywa maji haya ndani ya mwezi Disemba.” Alisema Meya huyo.
Aidha amezionya Kamati za Maendeleo ya Kata na Kamati za Maendeleo ya Maji kuhakikisha miradi hiyo inawanufaisha wananchi badala ya watu wachache wenye tamaa na kuwataka Madiwani na Wenyeviti kulisimamia hilo.
Katika ziara yake Meya huyo akiambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari ilishuhudiwa baadhi yake ikiwa kwenye hatua nzuri ikiwemo Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese ambapo ilishuhudiwa wananchi wakianza kuchota maji ya Kisima kilichokuwa kwenye hatua ya mwisho ya ujenzi wake.
Miradi hiyo ya Maji safi na salama ya kunywa ya visima ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwapatia maisha bora watanzania chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akizindua Mradi wa Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E, Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo (CHADEMA), Renatus Pamba.
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Kinondoni, Gonzalves Rutakyamirwa (kushoto) akimwelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (mwenye shati ya drafti) maendeleo ya mradi wa Maji safi na salama ya kisima unaotekelezwa kwenye Mtaa wa Mivuleni, Manzese, Dar es Salaam juzi wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwenye Kata tisa za Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Diwani wa Kata hiyo, Eliam Manumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kushoto) akiongozwa na
viongozi wa Kata ya Manzese kuelekea kwenye ukaguzi wa maendeleo ya
Mradi wa Maji Safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Mivuleni, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakazi
wa Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese, Manispaa ya Kinondoni, Dar es
Salaam wakichota maji ya mradi wa maji safi na salama ya kisima wa
Manispaa hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda (mbele kulia) akikagua kivuko
kinachounganisha Kata ya Sinza na Kijitonyama, Dar es Salaam wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Mendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji safi
na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E mwishoni mwa wiki.
Mkandarasi
wa Kampuni ya Drilling and Dam Construction Agency, Elzei Makaso
(kulia) akimelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto)
maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji safi na Salama ya Kisima katika
Mtaa wa Magomeni Dosi, Dar es Salaam wakati Meya huyo alipofanya ziara
ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki.

No comments:
Post a Comment