HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 2, 2013

WAANDISHI WA HABARI WA TANZANIA WAENDELEA NA ZIARA YAO NCHINI AFRIKA KUSINI

 Muongozaji wa Watalii kutoka Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini,Dada Pumla akienekeza jambo kwa baadhi ya waandishi wa habari na wadau kutoka Tanzania ambao wapo kwenye ziara ya wiki moja ya kutembelea vivutio mbali mbali vya utalii nchini Afrika Kusini.Hapa wakiwa nje ya Jengo la Kumbukumbu ya Wachimbaji na Waponda mawe wa Zamani,lililopo katika Hifadhi ya Gold Reef City,jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini.
Mashine za zamani za kuponda mawe zilizopo nje ya Jengo la Kumbukumbu ya Wachimbaji na Waponda mawe wa Zamani,katika Hifadhi ya Gold Reef City.
 Waandishi wa habari na wadau kutoka Tanzania wakiendelea kutembelea hifandhi hiyo ya Gold Reef City,jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini.
 Wanahabari wa Tanzania wakiwa kwenye Hifadhi ya Gold Reef City,jijini Johannesburg,nchini Afrika Kusini.toka kulia ni Frank Amani (The Citizen),Atuza Nkulru (The Gurdian),Sheria Ngowi (Mbunifu wa Mitindo na Blogger),Othman Michuzi (Blogger kutoka Michuzi Media),Hellen Kiria (kutoka Kampuni ya Frontline) pamoja na Anganile (Bang Magazine).
 Katika tembelea tembea yetu ndani ya Jiji la Johannesburg,tulifanikiwa kufika ilipo Nyumba ya Mzee Nelson Mandela iliopo Maeneo ya Oldman na kufanikiwa kuweka mawe yenye michoro na maandishi ya kumtakia heri na fanaka ambapo tuliyakuna mengine mengi yakiwa kwenye Bustani iliopo nje ya nyumba yake hiyo.
 Hii ndio Nyumba anayoishi Mzee Mandela mpaka hivi sasa ikiwa na Ulinzi mkali.
 Wadau Sheria Ngowi na Suleiman Khamis wakiwa kwenye bustani iliopo nje ya Nyumba ya Mzee Mandera.
Moja ya jiwe lenye ujumbe kwa Mzee Madiba.
 Mdau Sheria Ngowi akiwa kapozi
 Tukiwa ndani ya Jozi Treni ikiwa ni sehemu ya Utalii wetu katika maeneo mbali mbali nchini Afrika Kusini.
Mie,Hellen Kiria na Anganile.
 Pozzzzzz kwa picha na Wachekeshaji waliopo ndani ya Gold Reef City Park.
 Siku moja moja sio mbaya ni Mie kupozz kwa picha sehemu kama hizi,sio kila siku wao tuuuuuuu.....
 Mdau Atuza Nkurlu nae hakucheza mbali na taswira hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad