Watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wamepata Mwenyekiti mpya wa TUGHE katka uchaguzi uliofanyaka nchi nzima ili kujaza nafasi kadhaa zilizokuwa wazi.
Nafasi hizo ni pamoja na ile ya Mwenyekiti ambayo ilikuwa wazi kufuatia mwenyekiti aliyekuwepo Bwana Baraka Maduhu kujiuzulu baada ya kukabidhiwa majukumu mapya ya kikazi.
Nafasi nyingine ni ya Mwenyekiti Kamati ya Wanawake, mweka hazina na wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu ya TUGHE.
Katika uchaguzi huo Bwana Gabriel Ishole ameibuka kuwa mshindi wa nafasi ya mwenyekiti na kuwashinda wagombea wengine saba.
Akizungumza baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo Katibu wa TUGHE mkoa wa Ilala Bwana Gaudence Kadyango amempongeza mwenyekiti mpya na wajumbe wa kamati na kuelezea matarajio yake kuwa ushirikiano mzuri uliojengeka baina ya Tawi la TUGHE la NHIF na ofisi yake utaendelezwa kwa faida ya wafanyakazi na utendaji wa kazi wenye tija.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana Hamisi Mdee amesema amefurahishwa jinsi mkutano huo ulivyoendeshwa kisayansi ambapo matokeo ya kura za mikoani yalikuwa yakipokelewa kwa njia ya mtandao na kutangazwa mara baada ya upigaji kura, hatua ambayo imeondoa uwezekano wa kulalamikia ucheleweshaji au uchakachuaji wa matokeo.
Aidha ameelezea matarajio yake kuwa uongozi mpya wa TUGHE tawi la NHIF utaendelea kushirikiana na Menejimenti ya NHIF ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuimarisha utendaji kazi kwa faida ya wanachama wa NHIF na watanzania kwa ujumla.
Viongozi wa TUGHE tawi la NHIF waliochaguliwa leo watadumu hadi mwaka 2015 ambapo uchaguzi mkuu utafanyika tena.
Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Hamis Mdee akifungua mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa TUGHE Tawi la NHIF leo.
Naibu Mkurugenzi na viongozi wengine wa TUGHE wakifuatilia matokeo ya mkoani yaliyotumwa kwa njia ya mtandao.
Wanachama wa TUGHE wakifuatilia kwa makini matokeo ya mkoani.
Wanachama wakiwa makini kufuatilia na kulinda kura zao
Wasimamizi wa kura za nafasi ya Mwenyekiti TUGHE wakihesabu kura zilizopigwa Makao Makuu.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Ilala Bw. Gaudence Kadiango akihitimisha uchaguzi huo


No comments:
Post a Comment