Katibu
Mkuu wa ITU ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia
Mawasiliano Duniani Dr. Hamadoun Toure akisikiliza Maelezo kutoka kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma. Kulia ni Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni
Waziri wa ICT wa Thailand.
Na Innocent Mungy – Bangkok Thailand
Tanzania inashiriki katika Kongano la TEHAMA la Dunia linaloandaliwa
na Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani
(ITU-International Telecommunications Union) linalofanyika katika jiji
la Bangkok nchini Thailand.
Kongano hilo lenye Kauli Mbiu ya Kuchochea Mabadiliko Katika
Ulimwengu wa TEHAMA, unashirikisha nchi wananchama wa ITU na wasio
wanachama, Makampuni ya Mawasiliano Duniani, Taasisi na wasimamizi wa
sekta ya Mawasiliano Pamoja na Serekali, wanashiriki Kongano hili katika
kipindi ambacho mabadiliko makubwa katika Sekta ya Mawasiliano.
Mabadiliko haya yanapelekea dunia kuwa na Changamoto ya Kuyakubali
Mabadiliko hayo na kukabiliana na Changamoto zake kwani faida za
mabadiliko ni kubwa kwa Jamii Habari duniani. Akizungumza jijini
Bangkok, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Prof. Makame
Mbarawa amesema Tanzania iko tayari kwa na imeshapokea mabadiliko na
imetekeleza mikakati ya kuhakikisha Tanzania inapokuwa mabadiliko bila
tatizo.
Aidha Mheshimiwa Mbarawa amesema Tanzania inatambua umuhimu wa
mabadiliko katika TEHAMA hususan kipindi hiki cha dijitali kwani ndio
njia pekee ya kuharakisha maendeleo ya watanzania kwa ufanisi.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Prof. John
Nkoma amesema Tanzania tayari mstari wa mbele kuhakikisha inachochea
mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili wananchi wafaidike
na huduma za Mawasiliano.
“Tuna mfumo mzuri wa usimamizi wa leseni za
muingiliano wa teknolojia, sheria na kanuni nzuri ambazo zinawezesha
mabadiliko katika TEHAMA kunufaisha watanzania. Tayari Tanzania imeingia
katika mfumo wa Utangazaji wa digitali na tunaendelea kuweka mazingira
mazuri ya kuwepo kwa huduma nyingi zaidi kurahisisha maisha ya
watanzania”. Amesema Profesa Nkoma.
Taasisi kadhaa toka Tanzania zinashiriki
Kongano hili kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na W ziara ya Afya,
Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia, DTBi ya wavumbuzi na wagunduzi,
NICTBB inayosimamia mkongo wa Taifa, MaxCom.
Kongano hili linafanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 19 – 22 Novemba
2013. Tanzania inashiriki na kauli Mbiu ya nchi “Tanzania: Africa
Strategic ICT Hub”. Pamoja an Kongano pia yako Maonesho ya ICT yenye nia
ya kuonesha jinsi nchi zinavyochochea maendeleo kwa raia wake kupitia
TEHAMA.
Banda la Maonesho la Tanzania limevutia watu wengi wanafikia
kujifunza jinsi Tanzania imeweza kuchochea mabadiliko katika TEHAMA na
jinsi wananchi wanafaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa nchini.
Aidha Baadhi ya Taasisi zinazoshiriki zinaangalia uwezekano wa
kuchochea zaidi upatikanaji wa huduma zao kwa kuwa na washirika katika
shughuli zao. Leo asubuhi Ujumbe wa Tanzania ulishiriki katika Mkutano
Maalum wa Wawekezaji Katika Sekta ya Mawasiliano ulioendeshwa na Naibu
Katibu Mkuu wa ITU Bwana Houlin Zhao.



No comments:
Post a Comment