HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 7, 2013

Pambika na Samsung yazinduliwa rasmi kukamilisha ndoto za wateja wa Samsung ndani ya msimu huu wa sikukuu

Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania,Bw. Kishor Kumar (kushoto) akionyesha zawadi kubwa ya gari aina ya Mitsubishi Pick-up mpya mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kulia ni Sylvester Manyara Meneja Mauzo Rejareja wa Samsung Tanzania. Mteja mmoja wa Samsung atajiondokea nyumbani na gari hilo litakalosheheni bidhaa mbalimbali kutoka Samsung katika droo ya mwisho ya Novemba 23, 2013 itakayofanyika katika eneo la Kibiashara la Mlimani City, Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania, Bw. Kishor Kumar akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa promosheni kabambe ya Pambika na Samsung inayolenga kuwazawadia wateja watakaonunua bidhaa za Samsung na kuzisajili zawadi mbalimbali kila. Tukio hilo limefanyika katika Duka la Samsung liliopo Quality Center, Dar es salaam.
Meneja Mauzo ya rejareja wa Samsung Tanzania Bw. Sylvester Manyara akionyesha bidhaa mbalimbali za Samsung zitakazoshindaniwa kwenye shindano la Pambika na Samsung katika uzinduzi wa promosheni hiyo iliyofanyika leo katika duka la Samsung Quality Center, Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad