HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 15, 2013

MWANA FA KUTINGA STUDIO ZA VOA KATIKA LIVE TALK LEO

MwanaFA3
Mwanamuziki maarufu wa kizazi kipya Hamisi Mwinjuma a.k.a Mwana Fa a.k.a Binamu ambaye hivi sasa yuko nchini Marekani kwa ziara maalum anatarajiwa kuwa mgeni katika kipindi cha Live Talk katika idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika (VOA). 

Kipindi hicho ambacho hurushwa moja kwa moja na radio washirika kinaanza saa moja na nusu saa za Afrika Mashariki na saa kumi na mbili na nusu jioni saa za Afrika ya kati na Washington itakuwa ni saa tano na nusu asubuhi . 

Katika matangazo ya Ijumaa hii VOA itazungumzia suala zima la Muziki wa Bongo Flava unakoelekea na changamoto zake kwa ujumla. Kipindi hiki kitarushwa kwa muda wa saa moja ambapo nusu ya kwanza itakuwa kwenye radio washirika na ili usikie kwa saa nzima ungana na VOA kwenye mtandao . www.voaswahili.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad