Maandamano kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yalivyofan yika mjini Moshi
Afisa uhusiano wa shirika la KWIECO ,Veronica Ollomi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili ,Jaji Aisha Nyerere wakati wa maonesho yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa YMCA.
Viongozi wa taasisi mbalimbali zinazoshiriki katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Jaji Aisha Nyerere.
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Jaji Aisha Nyerere akitoa hotuba katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa YMCA mjini Moshi.
Na Dixon Busagaga,Moshi.
TAARIFA
zinaonesha kuwa Mkoa wa Manyara unaongoza kwa ukeketaji hapa nchini
ambapo takwimu zinaonesha kuwa kati ya Wanawake 100 wanaotoka katika
mkoa huo 71 wamefanyiwa ukeketaji.
Akitoa
taarifa za utafiti huo katika siku ya uzinduzi wa Maadhimisho ya
kimataifa ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zinazofanyika
kikanda mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, Mkurugenzi wa Mtandao wa
kuelimisha Jamii juu ya madhara ya Ukeketaji (NAFGEM), Francis Selesini
alisema kuwa tafiti hiyo inaonesha kuongezeka kwa vitendo vya
ukeketaji.
Selasini
alisema katika Utafiti huo uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na
shirika la kimataifa linaloshughulika na na watoto (UNICEF) kuhusu
athari ya vitendo vya ukeketaji, taarifa zinaonesha kuwa Mkoa wa Manyara
unaongoza kwa matukio ya ukeketaji ambapo kati ya wanawake mia moja, 71
wamekeketwa.
“Tafiti
mbambali zilizofanywa zinaonesha matukio ya ukeketaji kuongezeka hasa
katika Mkoa wa Manyara ambako kati ya wanawake mia, 71 kati yao
wamekeketwa, hili ni tatizo kubwa sana,” alisema Selasini.
Mkurugenzi
huyo alisema kuwa katika msururu huo pia imebainika kuwa mkoa wa Dodoma
ambayo ni makao makuu ya Tanzania Inafuata ambapo kati ya wanawake mia
moja, taarifa zinaonesha 60 kati yao wamefanyiwa kitendo hicho cha
kikatili.
Aidha
kuhusu Taarifa za kikanda Selesini aliitaja Kanda ya Kati inayoundwa na
mikoa ya Singida na Dodoma, kuwa kinara wa vitendo vya ukeketaji wa
wasichana ambapo kati ya wasichana mia moja, taarifa zinaonesha kuwa 50
kati yao kufanyiwa vitendo hivyo.
Kanda
ya Kaskazini, inayoundwa na mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Tanga na
Manyara, ni ya pili kwa matukio ya hayo ambapo kati ya wanawake mia
moja, 35 wamefanyiwa vitendo vya ukeketaji.
Hata
hivyo moja ya sababu za kukithiri kwa matuki hayo Mkoani Manyara, mkoa
unaoundwa kwa asilimia kubwa na Jamii ya Wafugaji, ilidaiwa kuwa ni mila
na Desturi ya watu wa maeneo hayo ambao wengi wao ni jamii ya Kimaasai
ambapo Ukeketaji kwa imani zao inaonekana kama sehemu ya mila na Desturi
na bila ya kufanya hivyo mwanamke huchukuliwa kama Mtu ambaye bado
hajakomaa.
Changamoto
nyingine zinazokabili mapambano ya kupinga ukatili huu ni swala la
Mfume Dume ambayo kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha kuongezeka kwa
Ukeketaji kwani wanawake wa maeneo hayo huwa hawana sauti ya kuzungumza
na kukemea kile ambacho wao wanakiona kama kikwazo kwao.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

No comments:
Post a Comment