Baadhi ya waokoaji wa jeshi la zimamoto wakiwa katika zoezi la uzimaji wa moto wa ndege katika eneo maalumu kwa ajili ya zoezi hilo,yaliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.Mazoezi hayo yamewashirikisha wanafunzi 22.
Ndege bandia ikitayarishwa kwa zoezi la kuzima moto wa ndege uliofanyika tarehe jana kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya zoezi hili jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpongeza Protacy Lichenjele(kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha uaminifu,kwani kitendo cha askari huyo kurudisha fedha baada ya kugundua amezidishiwa ni kitendo chenye kuhitaji moyo na uzalendo wa kuigwa.
Naibu Kamishna Jenerali wa jeshi la Zimamoto Tanzania Luteni Kanali Lidwino Mgumba akitoa taarifa ya mafunzo ya kozi ya zoezi la kuzima moto wa ndege jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Askari wahitimu wa Jeshi la zimamoto nchini wakifanya zoezi la kumkimbiza majeruhi kumpeleka hospitali baada ya kumuokoa kwenye ajali.zoezi hilo limeshuhudiwa na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.Dkt.Emannuel Nchimbi.(hayupo katika picha) jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Askari wa Jeshi la zima moto waliomaliza mafunzo ya kuzima moto wa ndege wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo katika picha) Mh, Dkt, Emmanuel Nchimbi, Nov, 21,2013, Wahitimu hao katika risala yao wamesema kwamba wamepata uelewa mkubwa utakaowawezesh a kufanya majukumu yao
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi(kulia) akipongezana na Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto nchini Piusi Nyambacha (kushoto) baada ya kumalizika hafla ya kozi ya zoezi la kuzima moto wa ndege kwa askari wa jeshi la zima moto jana jijini Dar es Salaam.
Picha na Mwanakombo Jumaa,MAELEZO.

No comments:
Post a Comment