HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 8, 2013

DKT BILALI AHUDHURIA KILELE CHA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MLIPAKODI JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa pili kwa kulipa kodi,Mwakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania, Paul Makanza, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa kwanza kwa kulipa kodi, Meneje wa Huduma za Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alois Qande Maleck, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Mkurugenzi wa TBC BW. Mshana akipokea Tuzo na Cheti kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi Tuzo na Cheti, Mwananchi Shujaa wa Kodi, Dkt. Shumba,aliyediriki kuwekwa ndani kwa kudai Risiti ya malipo yake ya chumba cha Hoteli katika moja ya hotel katika mikoa ya Tanzania Bara, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi zawadi na Cheti, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Ally Mshana, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene. Picha na OMR

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad