Wilfred Moshi na Mlima Everest, inazungumzia safari ya kusisimua na kutisha ya kijana shujaa wa Kitanzania anayefanya kazi ya upagazi kuhudumia watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.
Wilfred aliyaweka maisha yake rehani ili kuweka rekodi mpya kuwa Mtanzania wa kwanza kupanda Mlima Everest ambao ni mrefu kuliko yote duniani na kuiletea Tanzania sifa kubwa kimataifa.
Urban Pulse Creative Media, Freddy Macha wakishirikiana na Ubalozi wetu Uingereza wanakuletea habari hii ya kusisimua kwa majuma matano mfufulizo ili tuone na kujifunza kutokana safari yake ya hatari.
Asanteni,
Urban Pulse Creative, Freddy Macha na Ubalozi wa Tanzania, Uingereza

No comments:
Post a Comment