Mkurugenzi wa kampuni ya Faidika,Marion Moore (katikati), akisoma hotuba yake katika hafla ya kuwatangaza washindi watano walioibuka katika shindano la Faidika na Mikopo unaoboresha maisha, iliyofanyika kwenye Hotel ya Southern Sun Oktoba 24-2013 .jijini Dar es salaam, kulia kwake ni mratibu wa promosheni Dr. Ellen Otaru.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogondogo (SME),kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Consolotha Ishebabi, akielezea namna inayofaa kutumia mkopo, ili umnufaishe muuhusika na kukuza pato katika shughuli husika aliyoikopea (wakwanza kushoto), Bw.Emanuel Nnko, (wakwanza kulia),Bi Dina Binna ambao walikuwa majaji katika shindano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogondogo,
kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Consolotha Ishebabi akimkabidhi Tshs. 5,000,000 mshindi wa kwanza wa shindano la faidika na mikopo Bw. Vincent Tozzo mkazi wa iringa, mara baada ya kutangazwa mshindi.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda vidogo na Biashara ndogondogo, kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Consolotha Ishebabi akimkabidhi fedha kiasi cha Tshs. 3,000,000 milioni mshindi wa pili wa Faidika na mkopo Bi. Nisalalile Mwaipasi Mkazi wa Mkoa wa Tabora, mara baada ya kutanganzwa mshindi kwa kutumia mkopo vizuri na kumnufaisha yeye na jamii inayomzunguka, wakwanza kushoto ni Emanuel Nnko na wakwanza kulia ni Dina Bina ambao ndio walikuwa majaji wa shindano hilo.
Washindi wa shindano la Faidika na Mikopo pamoja na majaji na Wakurugenzi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo.




No comments:
Post a Comment