HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 25, 2013

BONANZA LA VITUO VYA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU LAFANA JIJINI DAR LEO

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kulia) leo katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila wakati wa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kushoto) akipiga mpira kuashiria kuanza kwa Bonanza la mchezo wa mpira wa miguu lililohusisha vijana kutoka katika vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam. Kulia anayeonekana kudaka mpira huo ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Diana Melrose (kulia) akikagua timu ya mpira ya FC Kigamboni kutoka kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Kigamboni kabla ya kuanza kwa michuano ya kuwania kombe katika bonanza lililovihusisha vituo 19 vya kulelea watoto walio katika mazingira magumu vya jijini Dar es salaam.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Uingereza,British Council, Baraza la Michezo Tanzania, na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo yakiendelea katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa British Council nchini Tanzania Bw.Richard Sunderland akikagua timu ya mpira ya kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Dogodogo leo katika viwanja vya michezo vya shule ya sekondari Kibasila.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (kulia) akimvisha medani kijana Juma Abdul wa kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Kigamboni leo jijini Dar es salaam.
Washindi wa jumla wa Bonanza hilo timu kutoka kituo cha kulelea watoto walio katika mazingira magumu cha Dogodogo wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Wizara ya Habari, Ubalozi wa Uingereza, Baraza la Michezo Tanzania,Right to Play Tanzania mara baada ya kunyakua kombe na medali mbalimbali.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad