Mtaa Kwa Mtaa Blog

Redd’s Uni-Fashion Bash yatikisha jiji la Mwanza

 Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 5 kwa Mshindi wa Kwanza wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Fahad Rajab (kutoka Chuo cha Mt. Augustine ya jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake,katika Tamasha lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.
 Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 7 kwa Mshindi wa Kwanza wa Ubunifu wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Dotto Elias (kutoka Chuo cha Biashara cha CBE jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake,katika Tamasha hilo lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.
 Mshindi wa kwanza wa Miondoko ya Mitindo,Fahad Rajab (pili kushoto) na Mshindi wa pili,Lucy Charles (kushoto) wakifurahia vitita vyao pamoja na wenzao.
 Picha ya pamoja.
Jaji Mkuu wa Redd's Uni-Fashion Bash,Dada Flora wa Flora Saloon (kushoto) akitangawa mshindi wa kwanza na wapili.kulia ni Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa,Andrew Mbwambo.
 Mkali Muziki wa Kufoka hapa nchini,Fareed Kubanda a.k.a Fid Q akitoa burudani kwa wakazi lukuki wa Jiji la Mwanza waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza kushuhudia Tamasha la Redd's Uni - Fashion Bash.
 Wabunifu wa Mavazi kutoka Vyuo mbali mbali vilivyopo Jijini Mwanza,wanaolioshiriki kwenye Tamasha la Mitindo lijulikanalo kwa jila la Redd’s Uni-Fashion Bash,wakiwa Jukwaani kabla ya kuanza kuwapitisha Wanamitindo waliovalia mavazi yaliyobuniwa nao.Tamasha hilo limemalizika Usiku huu kwenye,Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.


Picha mbali mbali za Wanamitindo hao wakipita jumwaani kuonyesha mavazi mbali mbali.

Majaji wakijadiliana jambo kabla ya kutangaza matokeo,kulia ni Dada Nurujan Maulid,Flora pamoja na Godman Kusolwa.
Wabunifu wa Mitindo walioingia hatua ya tano bora.
 Wadau mbali mbali wa Jiji la Mwanza wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza kushuhudia Tamasha la Redd's Uni - Fashion Bash.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget