HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 20, 2013

mwananyamala mabingwa wa kombe la meya wa kionondoni, wakabidhiwa bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi

Timu ya soka ya Mwananyamala jana iliibuka bingwa wa kombe la Meya wa Kinondoni na kukabidhiwa zawadi za bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo,Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba aliwaasa vijana hao kutumia vema zawadi hizo ikiwemo fedha na bajaj kwa kusaidia maendeleo yao ikiwemo kuboresha maisha yao. 

Makamba alimsifu Meya wa Manispaa hiyo,Mh Yusuph Mwenda kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanasaidia kuwaleta vijana pamoja na kudumisha mshikamano na amani baina yao. 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo,Mh Yusuf Mwenda alisema huo ni mwanzo tu wa kampeni yake ya kuweka safi manispaa yake ambapo kupitia michezo anawahamasisha wakazi wa manispaa hiyo kuweka safi mazingira yanayowazunguka.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (kushoto) akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Kionondoni. kushoto kwake ni Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda na Naibu Meya wa manispaa hiyo,Mh. Songoro Mnyonge.
Mshambuliaji wa Mwananyamala,Rashidi Kidebe (kushoto0 akiwania mpira na beki wa Kawe Kombaini Emmanuel Nengu, wakati wa mtanange wao wa fainali ya Kombe la Meya wa Kinondoni.
Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki ya matairi mawili kwa mwamuzi wa nje wa michuano hiyo.
Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (kushoto) akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya kawe issa kitasa ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Yusuph Mwenda (kulia) akipeana mkono na kocha wa timu ya kawe mara baada ya kuwakabidhi pikipiki kwa kuibuka washindi wa pili. anayeshuhudia (kulia kwake) ni Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba.
Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (katikati) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya kawe issa kitasa ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo. kulia ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Yusuph Mwenda.
Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (wa pili kulia) akikabidhi fedha tasilimu milioni 2 kwa nahodha wa timu ya kawe issa kitasa ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo. kulia ni Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda na Naibu Meya wa manispaa hiyo,Mh. Songoro Mnyonge (kushoto).
Kombe ndani ya Bajaj Mpya.
Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda (kulia) akikabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya mwananyamala, Ramadhani Kipanya baada ya timu yake kuibuka mabingwa wa michuano ya kombe la meya wa kinondoni.

1 comment:

Post Bottom Ad