HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 8, 2013

AMREF yaandaa chakulas cha hisani jijini dar

Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga kupitia kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania” siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy Mapunda, kulia ni Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso.
Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso (kulia) akisisitiza jamii nzima juu ya kutambua umuhimu wa kuwasomesha wakunga nchini ambapo azma hiyo itafanikiwa kwa kuunga mkono kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.
Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy Mapunda (kushoto) akiwashukuru washirika wanaoendelea kuunga mkono kameni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”, baadhi ya washirika hao ni ITV/Radio One, Clouds Media Group, Banki Kuu Tanzania (BOT), Serena hoteli, benki ya NBC, Toyota Tanzania Tanzania One, DSTV, PPF, TACAIDSWHO na MSD. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.

AMREF Tanzania kwa Ushirikiano na Benki M, wanaikumbusha jamii nzima kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili za kusomesha wakunga katika kampeni ya “Simama Kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania” siku ya tarehe 11 ya mwezi wa kumi, 2013, hapa Hoteli ya Serena.

Kwa Ushirikiano na Montage, AMREF imeandaa chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya kusaidia uboreshwaji wa afya ya mama na mtoto, na pia kuongeza idadi ya wakunga wenye utaalam nchini Tanzania. Nia ya AMREF ni kusaidia serikali ya Tanzania kufikia malengo iliyojiwekea ya millennia, MDG, hususani mpango wa tano, unaozungumzia uboreshwaji wa afya ya mama na mtoto.

Tuna furaha kuwaatarifu kwamba Mgeni wa Heshima katika chakula hiki cha hisani atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye ataongoza uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hii ili kupata wauguzi wakunga wa kutosha, na hivyo kuokoa maisha ya mama na mtoto. 

Fedha zilizopatikana mwaka uliopita zimeweza kusomesha wakunga 10 mkoani Tanga, hususani wilaya ya Kilindi, na zaidi ya wanafunzi wapatao 70 kutoka Mtwara, na Simiyu wanatarajiwa kwenda kwenya mafuzo ifikapo mwezi wa Novemba, 2013. Wanafunzi wengi zaidi kutoka pande mbalimbali za Tanzania watapata mafunzo kama fedha za kutosha zitapatikana.

Tunawaomba Watanzania wote, wake kwa waume kuungana na kusaidia uchangishwaji wa fedha katika mpango huu ambao utaendelea mpaka 2015.
Michango ya kusaidia kampeni hii inaweza kupokelewa kupitia njia zifuatazo:
  • Mpesa number +255 752 167286
  • Tigo Pesa  +255 716032441
  • National Bank of Commerce, Makao Makuu akaunti namba 011103000458

Tunapenda kuwashukuru washirika wafuatao, ITV/Radio One,  Bank of Tanzania( BOT) , Serena Hotels, National Bank Of Commerce, Clouds Media Group, The Guardian Limited, Toyota Tanzania, TACAIDS, WHO, PPF, Commercial Bank of Africa,  Songas , Tanzanite One,  Serengeti Breweries Limited (SBL), Coca cola, DSTV,  MSD, Mikono Business Consult na Extreme Solutions.

AMREF ina zaida ya miaka 57 barani Afrika, na imekuwa mstari wa mbele katika kuhakisha afya ya jamii mbalimbali inaboreshwa. Mwaka uliopita, tarehe 15 Mei, Tulizindua kampeni ya “Simama kwa ajili Ya Mwanamke wa Kiafrika”kwa ajili ya kusaidia kuboresha afya ya Mama na Mtoto. Tunahitaji  kuboresha viwango vya wakunga 2,800 na wataalam 1000 kwa kutumia njia mbalimbali ikiwamo na njia za mitandao ifikapo mwaka 2015.
Kwa  maelezo zaidi tafadhali wasiliana na Montage Limited KUpitia  0685 70 12 69, 0685 70 12 70, 0685 70 1289, au barua pepe: info@montagetz.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad