HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 8, 2013

AJALI YA MOTO KATIKA JENGO LA EXTELECOM, MAKAO MAKUU YA KAMPUNI YA SIMU TANZANIA (TTCL)

Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) inaarifu umma kuwa tarehe 7 Octoba, 2013 majira ya saa 11:45 asubuhi palitokea ajali ya moto ghorofa ya sita katika jengo la Extelecoms, mtaa wa Samora mahali yalipo makao makuu ya TTCL. Uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha moto huo unafanyika.

Tunashukuru kwa jitihada za wafanyakazi wa TTCL na vikosi vya zimamoto vya Halmashauri ya Jiji na Ultimate Security zilizofanikisha kudhibiti moto huo na hivyo kuzuia madhara kwa Kampuni na wapangaji wanaotumia jengo hilo.

Tunapenda kuwathibitishia wateja wetu kuwa huduma za TTCL kwa wateja wake hazikuathirika kwa namna yoyote ile na TTCL inaendelea kutoa huduma zake kama kawaida.

Tunawashukuru wote hususani wateja wetu waliotupigia simu kutaka kujua usahihi wa tukio hili na kwa kututhibitishia kuwa huduma zetu zimeendelea kuwafikia bila matatizo yoyote. Tunapenda kuwahakikishia kuwa TTCL itaendelea kutoa huduma zilizo bora zaidi kukidhi mahitaji ya wateja wetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad