Timu ya KMKM ya Kisiwani Pemba ikifurahia ushindi wake wa Ngao ya Jamii,mara baara ya kuifunga timu ya Chuoni mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini ya mchezo kwa kufunguma bao 1-1.Mchezo huo ulipigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar na kuwaniwa kwa Ngao ya Jamii,Waziri wa Serikali ya Mapinduzi asiekuwa na Wizara Maalum,Mh. Haji Faki Shaali (wa pili kushoto) akikabidhi Ngao ya Jamii kwa Nahodha wa timu ya KMKM,Ame Hamis Kibobeo mara baada ya kutwaa Ngao hiyo kwa kufunga timu ya Chuoni kwa mikwaju ya penati 5-4,katika mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.
Wachezaji wa KMKM wakipeana mkono na viongozi mbali mbali walikuwepo Uwanjani hapo.
Kikosi cha Timu ya Chuoni FC
Kikosi cha Timu ya KMKM.
Beki wa Timu ya Chuoni akijaribu kutaka kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya KMKM,Juma Mbwana (8) akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Timu ya Chuoni,Mwinyi Haji wakati wa Mchezo wao wa kuwania Ngao ya Jamii,uliochezwa jana Usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.hadi mwisho wa mchezo timu ya KMKM ilishinda kwa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati.
Mchezaji wa timu ya KMKM akiondoka na mpira.
Hatari langoni mwa timu ya Chuoni.
Goooooo........hii ndio penati ya mwisho ya timu ya KMKM iliyowapatia Ushindi na mpaka kunyakua Ngao ya Jamii.
Meneja Masoko wa Kinywaji cha Grand Malt,Fimbo Butallah (kushoto) akizungumza machache kabla ya kuanza kwa mechi hiyo.
Makamu wa Rais wa ZFA (Pemba),Ali Mohamed (kulia) akieleza jambo mbele ya Mgeni Rasmi na viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya KMKM na Chuoni,uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.
No comments:
Post a Comment