Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Uchunguzi wa Matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari Polisi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na tukio la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutumika katika uhalifu (ubebaji bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Polisi Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha na Mauaji ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la Polisi. Kutoka kushoto (waliokaa) ni Katibu Mkuu hiyo, Mbarak Abdulwakil, anyefuata ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Taarifa hiyo ameitoa katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Thursday, August 22, 2013
Home
Unlabelled
WAZIRI NCHIMBI ATOA TAARIFA YA UCHUNGUZI HADHARANI LEO
WAZIRI NCHIMBI ATOA TAARIFA YA UCHUNGUZI HADHARANI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment