HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, August 11, 2013

Profesa Maji Marefu ashiriki kusimamia uchimbaji wa kisima cha Maji

Mbunge wa Korogwe vijijini Mh. Stephen Ngonyani 'Profesa Majimarefu', akitazama gari linalochimba kisima katika kijiji cha Magamba-Kwalukonge huku mtaalamu wa maji akimpa maelezo.
gari la Kampuni ya Sum-hidrogeo Works likichimba kisima katika kijiji hicho.
Mbunge wa Korogwe vijijini Profesa majimarefu (wa pili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za mchanga katika eneo la awali lililochimbwa mita 120 lakini maji hayakupatikana aliye karibu yake kulia ni Opareta wa gari la kuchimbia Sathi Reddy.
hakukuwa na mchezo hata kidogo kutokana na shida ya maji, wazee nao waliacha shughuli zao na kufuatilia namna ukombozi wa maji utakavyopatikana kama ambavyo wazee hawa mke na mume wakifuatilia tukio hilo.

Na Mashaka Mhando,Korogwe

MBUNGE wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani ‘almaarufu Profesa Majimarefu’, kwa siku tatu mfululizo amekuwa akikesha katika kijiji cha Magamba Kwalukonge kusimamia uchimbaji wa kisima ili kutatua kero ya maji inayowakabili wananchi wa kijiji hicho.

Mwandishi wa Habari hizi, alimshuhudia mbunge huyo maarufu kwa jina la Profesa Majimarefu, akishinda na wananchi wake wakifuatilia uchimbaji wa kisima hicho unaofanywa na kampuni ya Sum-Hidrogeo Works ya Jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, eneo ambalo lilipangwa na wataalamu wa maji kuchimbwa halikuwa lenyewe na hakukuwa na mtu yeyote aliyetajwa kuonesha eneo lisilopangwa ambalo mkandarasi huyo alipochimba na kufika urefu wa mita 120, hakukuwa na maji yaliyotoka.

Mbunge huyo baada ya kuona mkandarasi amechimba umbali huo huku maji yakiwa hayana dalili kupatikana, aliamua kushika chombo kinachopima maji kisha kuyatafuta katika eneo jingine ambalo aliwahamisha wataalamu hao ambao walichimba mita 103 wakapata maji.

“Tunamshukuru mbunge wetu tumepata maji katika kijiji chetu tunalazimika kulala nje ya nyumba zetu kutafuta maji lakini sasa tunafurahi kupata maji haya,”alisema Mwanaisha Lusewa.

Akizungumza mara baada maji kupatikana mbunge huyo alisema kuwa ameweza kutatua kero hiyo ya maji katika kijiji hicho baada ya kupata msaada wa kiasi cha shilingi milioni 20 kutoka kwa kada wa CCM Jaffer Sabodo kati ya shilingi milioni 41 alizompa.

Alisema amepata msaada wa kiuchimbiwa visima viwili katika kijiji hicho na kingine cha Kijango kilichopo kata ya Magoma msaada ambao utamwezesha kusaidia maendeleo kwa wapiga kura wake.

“Tuwaache wengine wakipiga majungu ya kunichonganisha na wapiga kura wangu lakini mimi kazi yangu ni kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na ahadi zangu nilizowapa wananchi katika maeneo mbalimbali,” alisema Majimarefu.

1 comment:

Post Bottom Ad