Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Mtukwao’, akishea jambo na mmoja wa malaika Hospitali ya Taifa Muhimbili, upande wa saratani, Jumammosi iliyopita.
Mmoja
wa watoto wanaendelea na matibabu Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es
Salaam, akiwa bize na rangi wakati walipotembelewa na mchora katuni
Nathan Mpangala kupitia mradi wake wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu,
Jumamosi iliyopita. Mradi huo unaoshirikisha ndugu, jamaa, marafiki na
wachoraji wenzake, ulikwenda kuwafariji kwa kuwapa zawadi kisha kuchora
nao.
Marafiki wa Wafanye Watabasamu, walionesha tabasamu mapemaaaaa.
Sanaa inamchango mkubwa katika kupunguza msongo wa mawazo na kusahaulisha maumivu.
Mchora vibonzo wa ITV ambaye pia ni mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala akiwa na mchora vibonzo wa baadae.
NYUMBA TU, SIMPO. Akiendelezwa atakuja kuwa mchoraji mahiri wa majengo.
Mchoraji katuni wa gazeti la Nipashe, Abdul King O aka ‘Kaboka mchizi’, aliungana na Wafanye Watabasamu kuwatabasamisha malaika hawa.


.jpg)
No comments:
Post a Comment