Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttalah akizungumza machache wakati wa Uzinduzi kinywaji kipya cha Club 07 Vodka Lemon kilichozinduliwa hivi karibuni katika Ukumbi Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttalah akiwa na
mabalozi wapya wa kinywaji kipya cha Club 07 Vodka Lemon
kilichozinduliwa hivi karibuni katika Ukumbi Golden Jubilee Tower jijini
Dar es Salaam ambapo kinywaji hicho kimeingia sokoni rasmi.
Baadhi ya wadau waliohudhulia uzinduzi wa kinywaji kipya kiitwacho Club 07 Vodka Lemon wakiyarudi magoma mara baada ya kufanyika uzinduzi huo.
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imezindua kinywaji kipya kiitwacho Club 07 Vodka Lemon, ambacho kimeanza kupatikana nchi nzima kuanzia jana.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi wa Golden Jubilee Tower jijini Dar es Salaam juzi usiku, Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema kinywaji hicho kimezinduliwa ili kukidhi mahitaji ya soko hapa nchini.
“Kwetu TBL tuna furaha kubwa mno kutokana na kuanzishwa kwa kinywaji hiki, kwani tunaamini Watanzania wataendelea kupata kitu wanachopenda kwa muda wote.
“Kama ilivyo kawaida ya TBL kuzalisha bidhaa bora, ndivyo ilivyo pia kwa kinywaji hiki ambacho kina vigezo vyote na tunachoamini kitapendwa na wananchi wengi,” alisema.
Butallah alisema, Club 07 ni moja kati ya vinywaji bora zaidi kupatikana hapa nchini, kwani kimetengenewa katika ubora wa hali ya juu huku kikimfanya mnywaji asiwe na uchovu.
Akizungumzia zaidi kinywaji hicho, Butallah alisema kitapatikana nchi nzima, huku akitaka Watanzania wakipokee kwa mikono miwili na kukifanya kinywaji chao.
“Naomba Watanzania wote wakipokee kwa mikono miwili, kwani kama TBL tunataka kuendelea kuwapa bidhaa bora zaidi kuliko kampuni yoyote nyingine hapa nchini.”
Baadhi ya wadau mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo, walikisifu kinywaji hicho na kusema pamoja na kuwa na ladha nzuri, lakini pia ni kizuri huku kikiwa hakikuletei uchovu wa aina yoyote ile.
Club 07 ni moja kati ya vinywaji vya kimataifa na hapa Tanzania kitazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia (TBL).




No comments:
Post a Comment