HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 24, 2013

KATIBU MKUU KIONGOZI AZINDUA MASHINDANO YA SHIMIWI KWA MAZOEZI "MAKALI" JIJINI DAR LEO

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (Katikati), na viongozi wa juu wa Serikali na Mashirika ya Umma, akiongoza mazoezi ya kukimbia, ya wafanyakazi wa wizara, taasisi za serikali na mashirika yake, wakati wa uzinduzi wa bonanza la Mashindano ya SHIMIWI mwaka 2013 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Agosti 24, 2013. Zaidi ya michezo ishirini kushindaniwa katika mshindano hayo yaliyodhaminiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF na taasisi zingine yatafanyika Dodoma kuanzia Septemba 20 mwaka.
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue (Katikati), Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (Kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga, wakijinyoosha kwenye mazoezi "makali" yaliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi, Agosti 24, 2013, kuashiria kuanza kwa mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), yanayotarajiwa kuanza rasmi Septemba 20 mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Katikati), akiwa miongozi mwa wanamichezo waliokimbia umbali wa kilomita 3 kuashiria uzinduzi wa SHIMIWI mwak 2013 uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi Agosti 24, 2013. PPF inadhamini mashindano hayo yatakayofanyika Septemba 20 mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, akitoa hotuba kwa wanamichezo kutoka wizara, idara za serikali baada ya mazoezi makali asubuhi Jumamosi, Agosti 24, 2013 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana. Balozi Sefue aliyekuwa mgeni rasmi, awali aliongoza maelfu ya wanamichezo hao kukimbia umbali wa kilomite 3 na kufuatiwa na mazoezi ya kunyoosha viungo yaliyofanyika uwanja wa Taifa. Mashindano ya SHIMIWI mwak 2013, yatafanyika mkoani Dodoma ambapo michezo zaidi ya 20 kushindaniwa chini ya udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio akiwapasha habari waandishi siku ya Jumamosi Agosti 24, 2013, juu ya udhamini wa mfuko huo kwenye mashindano ya mwaka huu ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI), wakati wa uzinduzi uliofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wanamichezo walikimbia umbali wa kilomita 3 na kufanya mazoezi ya kukata na shoka yaliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Lulu Mengele.
Washiriki wakifanya mazoezi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi Agosti 24, 2013.PICHA NA K-VIS BLOG.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad