YULE mkali wa Muvi za kibongo na muongozaji wa muvi hizo,Jimmy Mponda a.k.a 'Jimmy Master' aliyewahi kutikisa
na mfululizo wa filamu za misuko iliyotoka sehemu ya kwanza hadi ya
tatu na Sasa amekuja na kitu kingine kipya kabisa kiitwacho Double J Final ambayo itazinduliwa rasmi hivi karibuni,huku ukiwa ni ujio wa mwisho kutoka baada
ya kutangulia na Doble J sehemu ya kwanza na yapili zilizotoka mwaka jana.
"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani
wanaopagawa na filamu za mapigano na kujawa mambo ya kipelelezi,"alisema J Plus.
Alisema Doble J Final pia ni ujio wake wa filamu nyingine ya mapigano na
kuna heka heka za kipelelezi ndani. J Plus aliyezoeleka sasa katika kuonesha
ubabe wa kufa mtu , kwa sasa ujio wake huo unatazamiwa kuingia sokoni mapema tu ,
mwezi ujao .
Pia Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy'
na pia wamo nyota wengine katika dulu la filamu kama Charles Magari , Hashim Kambi na
Veronica Viankero.
No comments:
Post a Comment