
Wazee hao walifika hapo ofisini kufikisha ujumbe wao kuhusu pensheni zao na masuala yao mengine ya msingi ambayo wanayadai kwa serikali.
Wamesema kuwa suala lao limeahidiwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM na limeshajadiliwa Bungeni ila cha kushangaza licha ya kuahidiwa na serikali bungeni lakini wazee hao wanasema hawajaona suala lao kwenye bajeti.
Kwa upande wake Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwajibu kuwa CCM itawasaidia katika suala hilo kwa kuwasiliana na serikali.
Wazee hao wamechukua pia fursa hiyo kupongeza Kamati Kuu kwa kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM .
No comments:
Post a Comment