Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakichezea mpira maalumu unaojaa nishati kila unapochezwa na nishati hiyo kutumika kuwasha taa ama kuchajia simu wakati wa uzinduzi wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete na Mgeni wake Rais Barack Obama wa Marekani,wakisikiliza maelezo juu ya mpira unaoweza kufua umeme.
Rais Barack Obama wa Marekani akipiga kichwa mpira huo wenye uwezo wa kufua umeme.
Rais
Barrack Obama wa Marekani na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
wakizungumza na watendaji wa kuu wa sekta ya umeme nchini.Kushoto ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mr.Maswi,mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam Sadik Meck Sadik na watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati kiongozi huyo wa Marekani
alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaofanywa na kampuni ya Symbion
power ya Marekani huko Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

Rais
Barack Obama wa Marekani akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na
Madini,Mh. Prof. Sospeter Muhondo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme
wa Symbion,uliopo Ubungo jijini Dar.
Rais Barack Obama wa Marekani akizindua rasmi mpango wa marekani wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment