HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 26, 2013

Marekani yaunga mkono upelekaji wa Brigedi Maalum DRC

 Taswira ya Ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  ulivyokuwa siku ya Alhamisi wakati wa mkutano uliojadili hali katika eneo la  Maziwa Makuu, mkutano huo ulihudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon,  Mwakilishi wake wa Maziwa Makuu  Mary Robinson, Mawaziri kutoka  nchi za Maziwa Makuu, SADC , Umoja wa Afrika,  EU, na Mkuu wa Banki ya Dunia aliyeongea kwa njia ya Video kutokea  Makao Makuu ya Banki hiyo jijini Washington.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza kwaniaba ya Serikali katika mkutano  huo ambapo alilitaka  Baraza Kuu la Usalama  Kudai ushahidi dhidi ya tuhuma na propaganda za uongo  ambazo zimekuwa zikielekezwa  dhidi ya Uongozi wa Juu wa  Brigedi  Maalum ambayo inaundwa na wanajeshi kutoka Tanzania, Afrika Kusini na Malawi.   Akasema  tuhuma hizo  zinazoipaka matope FIB bila  ya sababu zote za msingi zinalenga katika kudhoofisha mamlaka ya Brigedi hiyo na MONUSCO kwa Ujumla katika  kutafuta amani ya kudumu  DRC na kwamba Baraza  Kuu linawajibu wa kuwalinda wale wote ambao siyo tu wamejitolea kusaidia upatikanaji wa amani lakini pia wanabeba dhamana iliyoadhimu.  Tanzania ilikuwa kati ya nchi chache zilizoalikwa kuzungumza katika mkutano huo.
 Waziri  wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bw. John Kerry,  alizungumza wakati wa mkutano wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  uliokuwa ukijadili hali katika eneo la  Maziwa Makuu na  uungaji mkono Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa wa  Amani, Usalama na  Ushirikiano wa Maendeleo katika Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo na Maziwa Makuu.  Mkutano huo uliokuwa katika  ngazi ya Mawaziri umeandaliwa na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Julai. katika  hotuba yake, Waziri Kerry amesema  Marekani inakaribisha na kuunga mkono  upelekaji wa Brigedi Maalum ( FIB) katika eneo la Mashariki ya Kongo na  pia   inaunga mkono na itashirikiana na  nchi 11 zilizotia saini    Mpango  mpana wa kisiasa  ili  kuhakikisha   unatekelezwa na kufanikiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad