Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Bw. Charles Wakuling’anga akiwasilisha maoni ya kundi lake lililojadili eneo la haki za Binadamu katika Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika Halmashauri hiyo hivi karibuni.
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera,
Bw. Frederick Kabendwe akwasilisha maoni ya Wajumbe hao kuhusu Rasimu ya
Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano
uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni.
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Shinyanga,
Bi Caroline Shayo akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya katika
eneo la kuhusu Maadili ya Viongozi wa Umma katika mkutano uliofanyika
katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo hivi karibuni.
Mjumbe
wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Moshi Mkoani
Kilimanjaro, Bi. Jackline Moshi akichangia hoja wakati wa mkutano wa
kuijadili Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba katika Mkutano uliofanyika jana katika ukumbi wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo.
Wajumbe
wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida
wakiwa katika majadiliano ya kuipitia Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa
na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi
wa Halmashauri ya Wilaya hiyo hivi karibuni.

No comments:
Post a Comment