HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 23, 2013

Barclays Bank Tanzania yashirikiana na Nkwamira Sustainable life trust kusaidia vijana

Barclays Bank Tanzania leo imekabidhi hundi yenye thamani ya shillingi Millioni 120 kwa shirika lisilo la kiserikali lijukanalo kama Nkwamira sustainable life Trust ili kuweza kusaidia vijana waishio mitaani bila elimu au kazi.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam leo,Meneja wa mawasiliano na huduma za jamii wa Barclays Bank Tanzania Bi. Tunu Kavishe alisema “ utaratibu huu uliowekwa kati ya Nkwamira na Barclays utafanyika katika mikoa miwili ambayo ni Dar-es-salaam na Morogoro na itawapa vijana fursa wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 kuweza kupata nafasi za kujiendeleza kwa kupitia mafunzo ambayo yatagusa mada mbali mbali kama vile ukosefu wa ajira, uwezo wa kuwa wajasiriamali na kuweza kuendesha biashara zao pamoja na mafunzo ya kifedha.

Aliongeza “ mpango huu utawashirikisha vijana 60 kwa mkoa wa Dar-es-salaam na vijana 40 kwa mkoa wa Morogoro kupitia mitihani mbalimbali ambayo itaendeshwa na wataalamu wa biashara na fedha kutoka vyuo vikuu vya Tanzania. Wataalamu hao watawachuja vijana hao mpaka watakapopatikana washindi wawili.

Akiongea kwa niaba ya Nkwamira sustainable life trust, Mkurugenzi wa shirika hilo Bi. Noreen Mazalla alisema “ msaada ambao Barclays wameweza kutupatia ili kuendeleza vijana ni mkubwa na utaenda mbali sana kuwasaida vijana hawa, tunaahidi kuuendeleza vizuri na kuweza kupata vijana ambao wataweza kuutumia msaada huu vizuri”.

Barclays kupitia mpango wake wa kusaidia jamii unaangalia vijana waishio mitaani wasiokuwa na uwezo wa kujiendeleza kielimu au kupata kazi kutokana na kutokuwa na elimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad