BENKI ya Wananchi Mwanga (MCBL) iliyopo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro hivi karibuni imetangaza kupata faida ya Shilingi Milioni 74 kabla ya kodi kwa mwaka ulioishia Desemba 31, 2012.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya MCBL, Bw. Abby Y. Ghuhia, katika Mkutano Mkuu wa Wanahisa (AGM) 2013 uliofanyika makao makuu ya benki hiyo iliyopo wilaya ya Mwanga.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa: “MCBL imepata faida ya Shilingi Milioni 74 kabla ya kodi kwa mwaka Desemba 31, 2012. Malengo ya faida kabla ya kodi katika benki yetu hayakufikiwa kwa Shilingi Milioni 45 asilimia 38% kutokana na riba za amana kutoka vyombo vingine vya fedha kupanda. Gharama za riba zilikuwa zaida ya malengo kwa Shilingi Milioni 163 asilimia 48%.”
Aidha, Bw. Ghuhia alisema kuwa Amana kwenye Benki ya Wananchi Mwanga (MCBL) zimeongezeka kwa Shilingi Milioni 1,844 ambayo ni sawa na asilimia 38% kutoka Shilingi Milioni 4,917 ilivyokuwa mwaka 2011 na kufikia Shilingi Milioni 6,762 mwaka 2012.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa “hatua hii ya ongezeko la amana kwenye benki yetu inatokana na mikakati kamambe ya Benki hiyo ya kuongeza wateja, amana na umiliki wa soko nchini Tanzania.”
Bw. Ghuhia aliongeza kuwa, Amana za benki yake, ziliongezeka na kuzidi malengo kwa Shilingi Milioni 226 ambayo ni sawa na asilimia 3%, hivyo kuwezesha malengo ya ukopeshaji kufikiwa na kupitwa kwa Shilingi 619 sawa na asilimia 14%.
MCBL katika mwaka huu 2013, imejipanga ili kuongeza amana, mikopo, mapato, kudhibiti gharama na mikopo chechefu.
Ili kufanikisha Mpango Kazi (Business Plan) huo wa miaka mitano 2013-2017, Bw. Ghuhia, alisema kuwa MCBL inategemea kuongeza amana, mikopo, hisa kupitia vituo vya huduma ilivyofungua Moshi, Same, Kileo na baadae katika miji ya Hedaru, Njia Panda, Ugweno na Usangi.
Aidha, Mtaji wa hisa wa Benki ya Wananchi Mwanga (MCBL) umeongezeka kutoka kiasi cha Shilingi Milioni 503 hadi kufikia Shilingi Milioni 555 sawa na ongezeko la Shilingi Milioni 52 (10%). “Malengo ya mtaji wa hisa hayakufikiwa kwa Shilingi Milioni 56 ambayo ni sawa na asilimia 9%,” alisema Mkurugenzi huyo wa MCBL.
Bw. Ghuhia, alisema kuwa jumla ya mtaji imeongezeka kutoka Shilingi Milioni 1,018 hadi kufikia Shilingi Milioni 1,086 ambayo ni sawa na ongezeko la Shilingi milioni 68, sawa na asilimia 7. Mtaji halisi (core capital) umeongezeka kwa Shilingi Milioni 53 ambayo ni sawa na asilimia 6% kutoka Shilingi Milioni 851 mwaka 2011 hadi Shilingi Milioni 904 mwaka 2012.
Mkurugenzi huyo alieleza pia kuwa, rasilimali za benki zimeongezeka kwa Shilingi Milioni 1,426 sawa na asilimia 22% kutoka Milioni 6,565 mwaka 2011 hadi Shilingi Milioni 7,992 mwaka 2012. “Rasilimali za benki yetu (total assets) zilizidi malengo kwa Shilingi Milioni 68 ambayo ni sawa na asilimia 1%,” alisema.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCBL, Bw. Epaineto Toroka, kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Bw. Ibrahim Sehushi, alisema kuwa malengo ya mapato ya riba ya mwaka 2012 hayakufikiwa kwa Shilingi Milioni 139 (12%) kutokana na mikopo inayopitiliza muda wake kulipwa (mikopo chechefu).
“Matumizi yote kwa ujumla yalikuwa chini ya malengo kwa Shilingi Milioni 69 (7%) ingawaje gharama za uendeshaji zilikuwa juu kutokana na kupanda kwa mafuta, umeme na ufuatiliaji wa mikopo,” alisema Bw.Seushi.
Aidha, Bw. Seushi lisema kuwa kutokana na matokeo ya mwaka 2012, MCBL imeweka malengo yakuhakikisha kwamba kwa mwaka 2013, Amana, inaongeza kwa Shilingi Bilioni 381 ( 6%) na kufikia Shilingi Bilioni 7.14 kutoka Shilingi Bilioni 6.76.
“Hadi kufikia mwezi Mei 2013 tumekwishafikisha kiasi cha amana za Shilingi Bilioni 7.82 ambayo ni sawa na ongezeko la Shilingi Bilioni 1.74 (28%). Hivyo, tunawaomba Wanahisa kuongeza amana ili kunufaika na faida kubwa tunayolipa kutegemeana na kiwango cha fedha na aina ya amana,” alisema Bw. Seushi.
Aidha, Bw. Seushi, alisema kuwa Mikopo imekadiriwa kuongezeka kwa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.29 (25%) na kufikia Shilingi Bilioni 6.21 mwaka 2013 kutoka Shilingi Bilioni 4.92ilivyokuwa mwaka 2012.

No comments:
Post a Comment