Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Bwalo jipya la New Magunia la Askari wa Gereza Kuu Ukonga liliopo Jijini Dar es Salaam(Picha kwa Hisani ya Dawati la Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza)
======== ======= ========
Na Lucas Mboje na Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza
Katika mpango makati wa Jeshi la Magereza Nchini kuhakikisha Maofisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Magereza wanapata sehemu za kuburudika baada ya saa za kazi, Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja amekamilisha ujenzi na kuzindua Bwalo jipya la New Magunia la Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam.
Bwalo hili limeasisiwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam wa Wakati huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Nusu Rupia pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Gereza la Ukonga wa Wakati huo, Mrakibu Msaidizi Mwandamizi wa Magereza W. Moshi Kati ya mwaka 1994 na 1996 lakini lilishindikana kumalizika kwa sababu mbalimbali.
Kufuatilia uteuzi wa safu Mpya ya Uongozi wa Jeshi la Magereza Nchini ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja aliteuliwa kuliongoza Jeshi hilo sambamba na Makamishna watatu ambao ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile, Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Ally Malewa na Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga kwa pamoja wameshirikiana kukamilisha ujenzi wa Bwalo Hili.
Jumla ya zaidi ya Tsh. 37 Milioni zimetumika kukamilisha ujenzi wa Bwalo hilo la New Magunia. Aidha, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Joel Bukuku ametoa Huduma ya Televisheni pamoja na Dishi la Dstv kwa ajili ya kuangalia mpira na matukio mengine ya kidunia.
Akizungumza na Maafisa na Askari wa Mkoa wa Dar es Salaam ameahidi kuendelea kujenga na maeneo jirani yaliyosalia ikiwa ni sambamba na ujenzi wa Hosteli kwa ajili ya matumizi ya Maofisa na Askari watakaokuja Mkoa wa Dar es Salaam kikazi toka maeneo mengine Nchini ili wapate mahala pa kulala bila usumbufu.

No comments:
Post a Comment