HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 26, 2013

taswira tofauti tofauti kutoka jiji la Accra nchini Ghana

Nani alikudanyanya kuwa 'u-machinga" ni biashara za vijana wa kiume pekee, pengine kakosea!!! kina dada wa Ghana kati kati ya barabara wakichangamkia walaji wa bidhaa mbalimbali katika mataa ya Barabara Kuu, Highway, ya kuelekea mji wa Kumasi, jijini Accra.
National ya Ghana- Uwanja wa Kimataifa wa Mpira wa Ghana-Accra, wakati wa wiki sehemu ya maegesho ya magari inatumika vilivyo kuingiza kipato ili kuuweka katika hali safi muda wote. Sio kusubiri "makusanyo" siku ya mechi.
Waharibifu wa miundo mbinu ya Umma wametapakaa kila kona !!! mfuniko wa shimo la maji taka ukiwa umeota mbaya "ibiwa" na kuacha shimo kubwa kati kati ya barabara na kuwapa kazi ya ziada watumiaji picha imepigwa Mitaa ya Kaskazini ya Karneshie jijini Accra.
Kiota cha Movenpick-Ghana, hata Bongo ilikuepo!!
Matangazo ya biashara katika vyombo vya moto, mobile adverts,kwa sasa ndio yameshika kasi yanawafikia watu wengi kwa muda tofauti kama inavyooneka gari ya Kamisheni ya Kupambana na Ugonjwa na Virusi vya UKIMWI nchini Ghana.
Mlimani City ya jijini Accra, lah taswira za majengo yenye maduka makubwa Supermarkets -Shoprite, Game na Mr. Price.
W-store nao wamo katika msafara.Picha zote na Mdau Florence Lawrence.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad