HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 3, 2013

Mh. Lowassa achangisha zaidi ya sh. mil 300 katika wa harambee ya maendeleo ya Wilaya ya Nyasa

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache muda mfupi kabla ya kuendesha harambee ya kuchangia maendeleo ya Willaya mpya ya Nyasa iliopo Mkoani Ruvuma,katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre,Ilala jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi,Mh. John Komba akizungumza machache juu ya Wilaya hiyo mpya wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Willaya mpya ya Nyasa iliopo Mkoani Ruvuma,katika hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre,Ilala jijini Dar es Salaam.Mh. Komba ndio Mwenyeji wa harambee hiyo akishirikiana na Kamati ya Maendeleo ya Wilaya ya Nyasa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa,Ernest Kahindi akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa kuanza kuendesha harambee ya kuchangia maendeleo ya Willaya mpya ya Nyasa iliopo Mkoani Ruvuma,hafla iliyofanyika kwenye Viwanja vya Msimbazi Centre,Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea taarifa ya Wilaya hiyo mpya ya Nyasa,kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa,Ernest Kahindi.
Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk. Cyril Chami (katikati) akitoa ahadi yake ya kuchangia harambee hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Prof. Mbele wakati wa harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya mpya ya Nyasa.
Brigedia Jenerali Mstaafu,Julius Mbilinyi akitoa ahadi yake Mbele ya mgeni Rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi mchango wake kwa Mratibu wa harambee ya maendeleo ya Wilaya ya Nyasa iliyopo Mkoani Ruvuma ambapo yeye na marafiki zake walichangia kiasi cha Tsh.65 Millioni kwenye harambee iliyokusanya Zaidi ya Tsh. 300 milioni.
Madiwani wa Wilaya Mpya ya Nyasa wakizungumza na kutoa ahadi zao za michango.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad