HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 9, 2013

Travelport Tanzania yazindua huduma mpya ya kuuza tiketi za ndege

Mrurugenzi Mkuu wa Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew akizungumza mapema leo asubuhi wakati akifungua warsha ya uzinduzi wa huduma mpya ya "free* mobile travel itinerary app for iPhone and Android" inayomuwezesha mteja kupata huduma ya kununua tiketi ya ndege kwa kutumia simu ya mkononi.Warsha hiyo imefanyika leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya JB Belmont,Benjamin Mkapa Towers jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mipango wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Robert Maina akiwasilisha mada kwa wadau  na Mawakala wa kuuza tiketi za Ndege nchini wakati wa warsha iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mafunzo wa Travelport Tanzania,Rehema Issa akitoa mafunzo kwa Wadau na Mawakala wa kuuza tiketi za Ndege nchini juu ya huduma mpya ya "free* mobile travel itinerary app for iPhone and Android" iliyozinduliwa leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya JB Belmont Jijini Dar es Salaam.
MC wa Shughuli hiyo,Khadija Kellow akionyesha moja ya vipengele vya huduma hiyo mpya kwenye tangazo lililokuwepo kwenye ukumbi huo.
Katibu wa Chama cha TASOTA,Shamim Kermali akitoa neno kutoka kwenye chama hicho.
Baadhi ya Mawakala kuuza tiketi za Ndege nchini,wakiuliza maswali mbali mbali juu huduma hiyo mpya ya "free* mobile travel itinerary app for iPhone and Android" wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya Mawakala wa walioshiriki warsha hiyo wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikiwakilishwa ukimbini hapo.
Ofisa Mipango wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Robert Maina akielekeza jambo juu ya huduma hiyo mpya.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Travelport Tanzania,toka kulia ni Meneja wa Ufundi,Julius Haule,Ofisa wa Mahusiano na Mawasiliano,Omar Kazimoto pamoja na Ofisa Mipango wa Kampuni ya Travelport Tanzania,Robert Maina.
"Ukiwa na hii Tablet unapata huduma yetu vizuri sana" hivyo ndivyo asemavyo Omar Kazimoto wakati akimuonyesha mmoja wa wateja wa huduma hiyo.
Mrurugenzi Mkuu wa Travelport Tanzania,Eliasaph Mathew akifafanua jambo kwa mawakala hao.
Baadhi ya Mawakala wa walioshiriki warsha hiyo wakifatilia mada mbali mbali zilizokuwa zikiwakilishwa ukimbini hapo.

1 comment:

Post Bottom Ad