HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 11, 2013

TBL yakabidhi mradi wa maji kwa wananchi Wilayani Same

Kandarasi wa ujenzi wa mradi kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania TBL .Godwin Kalaghe wa kampuni ya Dr Gogo engineering limited ya jijini Dar es salaam akimkabidhi mkurugenzi wa mahusiano na sheria wa TBL Stephen Kilindo taarifa za kukamilika kwa mradi huo.
Mradi wa kisima cha maji kilichofadhiliwa na kampuni ya bia Tanzania katika kijiji cha Makanya wilayani Same chenye thamani ya shilingi milioni 51.6.Uwepo wa kisima hiki utasaidia kupunguza tatizo la maji hususani kwa wakazi wa Tambarare katika wilaya ya Same.
Mkurugenzi wa mahusiano na sheria wa kampuni ya bia Tanzania TBL Stephen Kilindo akisaidia kumbebesha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Makanya Asia Zuberi kuashiria uzinduzi wa mradi wa kisima hicho cha Maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad