HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 15, 2013

PPF yaendesha tamasha la kutangaza fao la elimu Wilaya ya Kinondoni jijini Dar

Mkuu wa Wilaya ya Kiondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana, (Aliyesimama), akitoa hotuba kwenye tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF kwenye viwanja vya chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam Aprili 13. Wengine pichani kutoka kulia, ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, na Meneja wa PPF kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akihutubia kwenye tamasha la kutangaza fao la elimu la mfuko wa PPF, Kanda ya Kiondoni jijini Dar es Salaam Aprili 13.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Watatu kulia), akimkabidhi zawadi Mwangalizi wa wanafunzi shule ya sekondari Loyola ya jijini Dar es Salaam, Herieth, wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini Aprili 13. Wanaoshuhudia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Wapili kulia), akimkabidhi zawadi mwanafunzi wa kidato cha tatu, shule ya sekondari Loyola, ambaye ni mmoja wa wanafunzi wanaosoma kupitia fao la elimu la mfuko huo, Jolen Nyonyi wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini Aprili 13. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Watatu kulia), akimkabidhi zawadi makamu mkuu wa shule ya sekondari Makongo jijini, Meja Mayeba, wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini Aprili 13. Wanaoshuhudia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (Kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio.
Mkuu wa Wilaya ya Kinodnoni jijini Dar es Salaam, Jordan Rugimbana (Kulia), akipena mikono na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Kanda ya Kinondoni, Zahra Kayugwa, mwishoni mwa tamasha la kutangaza fao la elimu la Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye viwanja vya chuo cha ustawi wa Jamii jijini mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akifurahia jambo na mcheza sarakasi wa kikundi cha sarakasi, Safi cha jijini Dar es Salaam, wakati wa tamasha la kutangaza fao la elimu la mfuko wa PPF, Kanda ya Kiondoni jijini Dar es Salaam Aprili 13.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Kushoto), akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, mwishoni mwa tamasha la kutangaza fao la elimu la mfuko wa PPF, Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad