HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 24, 2013

Mama Salma Kikwete kuwa mgeni rasmi katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 ya fao la elimu litolewalo na PPF

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Katikati), akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam. Mfuko wa Pensheni wa PPF huwalipia ada na mahitaji mengine watoto wa mwanachama aliyefariki baada ya kuchangia miaka 3 au zaidi. Kwa Mwaka 2012 peke yake Mfuko umewasomesha watoto 1333 katika shule 765 zikiwemo shule 315 za msingi na 450 za sekondari hapa nchini kwa kuwalipia kiasi cha shilingi millioni 682. watoto zaidi ya 400 wa Dar es salaam, wanaosomeshwa chini ya fao la elimu litolewalo na mfuko huo, wanatarajiwa kushiriki kwenye hafla ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa fao hilo Jumamosi hii kwenye ukumbi mpya wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa WAMA, Mke wa Rais, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Kushoto ni Meneja wa Michango wa Mfuko huo, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Operesheni wa mfuko huo , Cosmas Sasi
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Katikati), akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam.Mfuko huwasomesha watoto wa mwanachama aliyefariki kuanzia chekechea mpaka kidato cha nne baada ya mwanachama kuchangia miaka 3 na kuendelea. Mwaka huu 2013 Mfuko unatimiza miaka 10 tangu kuanzisha kwa fao la elimu mwaka 2003 ambapo hafla ya kusheherekea miaka 10 itafanyika tarehe 27/04/2013 kwenye ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa WAMA, Mke wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mama Salma Kikwete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad