HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 1, 2013

Wimbi la wizi wa Watoto laibuka mkoani Mbeya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,ACP Diwani Athuman

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Kamishna Msaidizi wa Polisi,ACP Diwani Athuman amewatahadhalisha wananchi wote wa Mkoa wa Mbeya kuwa makini na Mienendo ya Watoto wao pindi waendapo na warudipo shuleni na hata wawapo Michezoni,wahakikishe kuwa wanarudi Majumbani Maepema.

Amewataka wananchi hao kuwafundisha Watoto wao kutopokea zawadi au lifti kutoka kwa watu wasiowafahamu,kwani kufanya hivyo itasaidia kuwaepusha Watoto wao na vitendo vya wizi wa Watoto.

Kamanda Athuman ametoa tahadhali hiyo kutokana na kuibuka kwa wimbi la matukio ya wizi wa Watoto wadogo.

IFUATAYO NI TAKWIMU ZA WIZI WA WATOTO MKOA WA MBEYA

JANUARI – FEBRUARI 2013 WIZI WA WATOTO

MBEYA Matukio 2

- Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1 
- Watuhumiwa Me 1,Ke 1 [Wamepatikana]

MOMBA - Tukio 1

- Watoto walioibwa Ke 1 
- Watuhumiwa -Nil Amepatikana

KYELA - Tukio 1

- Watoto walioibwa Ke 1 Amepatikana

JANUARI – DESEMBA 2012 WIZI WA WATOTO

MBEYA Matukio 4

- Watoto walioibwa Me 3, Ke 1 
- Wamepatikana wote wazima 
- Watuhumiwa Me 3, Ke 1

RUNGWE - Kesi 2
- Watoto walioibwa 2, Me 1,Ke 1 
- Wamepatikana
 - Watuhumiwa Me 1,Ke 1

MBARALI - Kesi 1
- Mtoto 1
 - Amepatikana

Uchunguzi wa mashauri hayo bado unaendelea ili kubaini chanzo cha matukio hayo, yeyote mwenye taarifa kuhusiana na matukio haya azitoe kwenye vyombo vya ulinzi na usalama.

1 comment:

Post Bottom Ad