Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni hii
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt wakipokea heshima za nyimbo za Taifa pamoja na saluti ya mizinga 21 katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jioni ya hii.
Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake
Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt na mwenyeji wake wakifurahia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa uwanjani hapo.
Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt akipkea shada la maua.
Waziri mkuu wa Denmark Mhe. Helle Thorning-Schmidt akisalimiana na kinamama waliofurika uwanjani kumlaki. Picha na Freddy Maro - Ikulu.
No comments:
Post a Comment