HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 6, 2013

Kampuni ya Mabibo kuendelea kupambana na Wasambazaji feki wa Bia hapa nchini

 Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,James Rugemarila (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa Elkad 24,Mikocheni jijini Dar.Hali hii imekuja kutokana na kujitokeza kwa wafanyabiashara wanaoingiza baadhi ya bidhaa kwa njia za magendo, hali inayoikosesha serikali mapato kwa kiasi kikubwa. Wafanyabiashara hao wasiowaaminifu wamekuwa wakiingiza bia hiyo ya aina ya Windhoek kwa njia za magendo ili kukwepa kulipa ushuru halali wa serikali na kuikosesha mapato ambayo yangetumika katika miradi mingi ya maendeleo.Wengine pichani ni toka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Benedictor Rugemarila,Meneja Mkuu wa Mabibo,Neil Stainton pamoja na Mshauri wa Mambo ya Usalama na Sheria wa Mabibo,Kamala Stephen.
Meneja Mkuu wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Neil Stainton akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wakitoa taarifa ya uhalali wa usambazaji wa Bia za Windhoek zinazotengenezwa na Kampuni ya Namibia Breweries,leo kwenye Ukumbi wa Elkad 24,Mikocheni jijini Dar.Kulia ni Mshauri Mkuu wa Kampuni ya Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,James Rugemarila.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mabibo Beer,Wine & Spirits Tanzania,Benedictor Rugemarila akionyesha namba maalum (inayosomeka MB 66) iliopo kwenye chupa ya Bia ya Windhoek inayoitambulisha Kampuni yake kuwa ndio yenye uhalali wa kusambaza vinywaji hivyo hapa nchini.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad