HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 27, 2013

Watu wawili wauwawa kinyaka kwa tuhuma za kishirikina wilayani Makete

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe,RPC Flugecy  Ngonyani
Na Edwin Moshi,Mtaa kwa Mtaa Blog - Makete

Watu wawili wanaume wakazi wa kata ya Mlondwe wilayani Makete wameuawa kwa kukatwakatwa na mapanga na watu wasiojulikana kwa kuhusiswa na tuhuma za kishirikina.

Tukio hilo limetokea usiku wa jana machi 26, kutokana na wananchi wa eneo hilo kudai kuwa wamechoka na vitendo vya kichawi vilivyokuwa vikifanywa na watu hao ambao kwa sasa wote ni marehemu.

Akizungumza na mtandao huu mmoja wa wakazi wa kata hiyo ambaye akitaka jina lake litiwe kapuni alisema kuwa  kumeibuka wimbi la mambo ya uchawi katani hapo kwa muda mrefu ambapo pia vimeibuka vifo vya kutatanisha ambavyo wananchi hao wanashindwa kuvielewa.

“Juzi tu hapa tumekuta maiti ya mtoto kwenye vitindi, mtoto huyo alipotea kwenye mazingira ya kutatanisha siku kadhaa zilizopita lakini ndiyo hivyo, watoto wetu wanaisha hapa ndugu mwandishi, na katika chunguza yetu hao waliouawa ndiyo waliobainika kuwa ni wahusika wakuu” aliongeza mwananchi huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Ng’onde katani humo Bw. Leksadi Sanga amesema ni kweli amepata taarifa za kutokea kwa mauaji hayo ambayo yamewashitua wengi, ambapo pia pamoja na mambo mengine baadhi ya shughuli zimeathiriwa na mauaji hayo.

Amesema kutokana na kawaida ya misiba watu kusaidiana shughuli za hapa na pale jambo hilo limekuwa likisababisha shughuli nyingine zikiwemo za maendeleo katika vijiji vya kata husika kusimama kwa muda kutokana na misiba hiyo.

Jeshi la polisi wilayani Makete lilifika eneo la tukio kufanya upelelezi wa mauaji hayo ili hatua za kisheria zifuatwe ikiwemo kuwabaini wahusika wa mauaji hayo.

Hadi ripota wetu anaondoka eneo la tukio,alishuhudia polisi wakiwa wanaendelea na upelelezi wao na kuahidi kutoa taarifa kamili baada ya kufika wilayani.

Mtandao huu utakujuza zaidi kuhusu tukio hilo mara baada ya kupewa taarifa kamili na jeshi la polisi Makete.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad