HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 26, 2013

Mh. Lowassa aongoza maelfu kumzika Nyiti jijini Arusha leo

Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa ameongoza maelfu ya Wakazi wa mji wa Arusha na mikoa ya jirani katika mazishi ya mfanyabiashara na Kada maarufu wa CCM Mkoani Arusha,Marehemu Henry Nyiti,nyumbani kwake Tengeru Arusha .

Nyiti alifariki ghafla wiki iliyopita akiwa katika mgodi wake wa madini,Mahenge Mkoani Morogoro.

Wengine walioudhuria katika mazishi hayo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe,Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu,Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo,Mwenyekiti wa Chadema,Mh. Freeman Mbowe na Ridhiwani Kikwete.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongoza viongozi wenzake kwenda kwenda kuweka udongo kaburini.nyuma yake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Mh. Bernard Membe.
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP,Dr. Reginald Mengi naye akiweka udongo kaburini.
Waziri Mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka shada la muawa kaburini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad