HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 29, 2013

Up Date: Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wafika eneo la tukio la Jengo Kuporomoka

Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadcik akifafanua jambo kwa Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said cMeck Sadick shoto akiwa ameambatana na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya,kulia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mbunge,Mh Mbatia muda mfupi mara baada ya kufika na kujionea hali halisi ya jengo la Ghorofa lililoporomoka mapema leo asubuhi na kupelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa vibaya.,aidha shughuli za ukoaji zinaendelea kwani inadaiwa kuna watu wengi zaidi wamefunikwa na jengo hilo.
Rais Kikwete akiondoka eneo la tukio mara baada ya kujionea hali halisi ya tukio zima la kuanguka kwa ghorofa linalodaiwa kuwa na idadi ya ghorofa 16.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akipewa pole na Katibu wa NEC,Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.Dkt.ASha-Rose Migiro kuhusiana na tukio zima la kuanguka kwa jengo la Ghorofa mapema leo asubuhi,jijini Dar.
Wadau wakimwagia maji kijiko cha greda ili kurahisisha kuingia kwenye kifusi.
Wanajeshi wakiendelea na kazi ya uokoaji.
Bango la Mkandarasi.
Uokoaji ukiendelea.
Wanajeshi wakinyanyua moja pande la kifusi.
 Jengo la Jirani na lililoanguka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad