
Mkongwe
wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo almaarufu, Lady Jaydee usiku wa
kumkia leo alifanya uzinduzi wa video yake mpya (hiyo juu) aliyomshirikishja Mkongwe
Mwezake katika burudani hiyo, Joseph Haule ‘Prof. J’ Video ya Wimbo unaokwenda
kwa jina la ‘JOTO HASIRA’.
Jaydee
alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Longe uliopo Namanga
wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa
Burudani na muziki wa mwana dada huyo.
Uzinduzi
huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani
ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Pichani
juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida,
mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.kuona picha zaidi tembelea libeneke la Father Kidevu Blog.

No comments:
Post a Comment