Eneo Posta barabara ya Jamuhuri eneo ubavuni mwa Supermarketi ya Imaraseko likiwa limefurika maji kufuatia kunyesha mvua kwa muda mfupi hali iliyosababisha usumbufu kwa watumiaji wa eneo hilo.
| Watu mbalimbali wakipita kwenye dimbwi hilo la maji kwa kukanyaga juu ya kreti tupu za kuhifadhia Soda baada ya wajasiriamali kuziweka na kuwalipisha shilingi miamoja kwa kila mtu. |
| Kazi kwelikweli vijana wabunifu! |
| Mmoja wa vijana hao akiwazuia watu ili aweke vizuri vifaa vya kuvukia. |
| Magari nayo yalionja karaha ya mvua! |
| Eneo la Kariakoo nalo lilikumbwa na uhaba wa magari kutokana na mvua hiyo kusababisha magari mengi kuharibika na abiria kurundikana kwenye vituo vya mabasi. |

No comments:
Post a Comment