Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (wa tatu kushoto) akitoa taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dk. Nchimbi alisema hali ya ulinzi na usalama nchini kimsingi imendelea kuwa shwari isipokuwa kwa matukio machahe yaliyogusa hisia za watu kutokana na kutokuwa ya kawaida katika jamii yetu, na kuwa Serikali inayafanyia uchunguzi wa kina matukio hayo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama Mama Anna Abdallah
(mbele katikati) akifuatilia taarifa ya Hali ya Ulinzi na Usalama
iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi
katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam. Wengine ni wajumbe wa
Kamati hiyo na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment