Leo hii hapa jijini Dar kumenyesha mvua kubwa kiasi iliyopelekea kujaa maji kwa njia nyingi za maeneo mbali mbali,hali iliyopelekea kina sie tuanze kusaula viwalo vyetu na kuingia majini ili kuendelea na safari zetu.kikweli hali hii imekuwa ikintatiza sana mie hasa nikiwaza kwamba ni kwanini mvua kidogo tu hapa lakini maji lundo????hapo bado hujafika huko barabarani ambako nako gari hazisogei hata hatua moja.
aaahhh.... mie ndio nshaamua zangu kupiga chini viwalo na kuingia majini.
Hapa napo mambo ndio kama hivi.
Biashara ya Pweza kwa mdau huyu hata sijui kama itatoka leo.
Bodaboda inaendeshwa kwa staili ya miguu juu.
Jamaa wa Magazeti kaona isiwe tabu,acha akapaki tu mkoko wake.
No comments:
Post a Comment