HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 3, 2013

Hafla ya Siku ya Wanawake yafana sana jijini Dar leo


Mgeni Rasmi katika Hafla ya Siku ya Wanawake,Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akisoma hotuba fupi mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofayika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni mwelekeo wa kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimisha Machi 8 Duniani kote.
 Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa akisalimiana na mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda kwenye hafla ya Women's Celebration 2013 iliofanyika leo jijini Dar.
Muandaaji wa hafla ya Women's Celebration 2013 kutoka kampuni ya 8020 Fashions, Shamim Mwasha akipongezwa na Mgeni Rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda kwa kazi nzuri alioifanya ya kufanikiwa kuwakusanya wanawake wenzake na kujadili mambo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia na maendeleo kwa ujumla,hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.Hafla hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuelekea kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa Machi 8 Duniani kote.
 Mwimbaji mahiri wa miondoko ya taarab nchini,Khadija Kopa akitumbuiza mbele ya wageni mbalimbali waliofika kwenye hafla ya  wanawake (Women's Celebration 2013) iliondaliwa na kampuni ya 8020 Fashions,iliofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee VIP,jijini dar.
 Mke wa waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (pichani katikati) akijimwaya mwaya pamoja na Wageni waalikwa mbalimbai waliohudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh Angela kairuki akiwa sambamba na Mke wa waziri Mkuu Mstaafu,Mama Regina Lowassa wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijiri kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Mmoja wa Maofisa na Exim Bank ambao ndio wadhamini wakuu wa Hafla hiyo akijitambulisha. 
 Wageni waalikwa mbalimbali wakijadiliana mambo hapa na pale. 

2 comments:

  1. Hawa ndio wanawake wa Tanzania wengine aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa. Hata habari hawakuwa nazo...Hii ingetangazwa wakujitikeza wakajitokeza kushiriki sio wanawake wa vingozi tu na wenye wale wenye kujulikana tu.

    Lakini haishangazi, wanawake kubaguana ni kawaida. Hata wenye uongozi wa juu hilo huwa hawalioni.

    ReplyDelete
  2. Ndio hii kweli inayoitwa wanawake na maendeleo? kiukweli haijakaa vizuri ubaguzi Tanzania utaisha lini? wapo wengi wenye uwezo si wakubwa tuu viongozi wetu ebu muwe mfano bwanaaa!!!!!!!!! kaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad