Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi.
Wanariadha kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwamba wao katika mbio za
Nyika za Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Wakenya walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya
Mkimbiaji wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka huu upande wa
wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph alebeba Medali ya
Dhahabu.
Nafasi ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick
Kiagor, Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice
Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.


Aidha katika mbio za Kilometa 21, Kenya ilitamba tena kwa upande wa
wanaume baada ya wakimbiaji wake watatu kushika nafasi za juu ambapo Mshindi
alikuwa ni Silah Limo huku nafasi ya pili ikienda kwa Bernard Kiprotich na
nafasi ya tatu ikienda kwa Charles Ogari.
Mtanzania Dickson Marwa alinyakua nafasi ya nne na nafasi za tano na
sita zikenda Tena Kenya kwa wakimbiaji Peter Kusgei na Evans Taigey nafasi ya
saba ilishikwa na Mtanzania Stephano Huche na kuporwa tena na Kenya nafasi ya
nane iliyoenda kwa Patrick Wambugu aliyekimbia mbele ya watanzania wawili
waliofunga hesabu ya wakimbiaji kumi bora ambapo namba tisa alikuwa Said Makula
na kumi alikuwa Peter Sule.
Shangwe ya watanzania iliibuliwa na Mwana dada Sara Makera Ramadhan
baada ya kunyakua medali ya dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza mbele ya
mkenya Vicomi Chepkemoi huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mtanzania mwingine
Failuna Makanga.
Nafasi ya nne ilienda kwa Joyce Kiplimo wa Kenya aliyefuatiwa na
mwenzake Pauline Muchiri kasha Mtanzania
Catherine Tuku alishika nafasi ya sita na zilizosalia hadi nafasi ya kumi
zikienda kwa Nchi ya Kenya ambao ni Nancy Kotch, Jacinta Mboani, Florence
Cheruiyot na Phylas Jelagat.
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon
2013.
Wakimbiaji wa Kenya
wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio hizo.
Mfukuza Upepo kutoka Nchini
Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio za Kilimanjaro Marathon
akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha
Ushirika Mjini Moshi.
Eunice Muchiri akikimbia na kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42
Wanawake, katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo
hii leo katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza kukimbia Kilometa 21 katika mbio
za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na
kuwa kocha wa Kwanza wa Timu ya Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa
kwake miaka 10 iliyopita.

No comments:
Post a Comment