Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Lindi,Bi. Fortunata Raymond (kushoto) akikabidhi msaada wa mashuka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa,Bi. Agness Hokororo kwa ajili ya Hospital ya wilaya hiyo,Kulia Mkugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa,Bw. Mfune akishuhudia tukio hilo.
Wadau mbalimbali wakishiriki semina Kuhusiana na mfuko wa afya ya jamii CHF Wilayani RUANGWA.
Abdulaziz video,Ruangwa
MKUU wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi Agnes Hokororo amemtaka mganga
mkuu wa wilaya hiyo kuzitumia fedha za mfuko wa afya ya jamii
kununulia dawa na vifaa tiba ili kuondoa upungufu wa madawa
unazozikabili zahanati na vituo vya afya mara kwa mara katika wilaya
hiyo.
wito huyo ameutoa wakati alipokuwa anafungua mafunzo ya elimu ya
kata kwa kata kwa wadau na wanachama wa mfumo wa taifa bima ya afya
na jamii uliofanyika wilaya ruangwa jana.
hokororo alisema kuwa kero nyingi zinatolewa na jamii kuhusiana na
huduma za mbovu zinazotolewa kwenye baadhi ya vituo vya afya ,
zahanati, inasababishwa na watendaji wasio waadilifu katika sekta ya
afya kwa ukosefu wa dawa wilayani humo.
alisema wapo watumishi wachache wenye malengo ya kuvipaka matope
vituo vya kutolea huduma kwa sababu zao binafsi na imani potofu kuwa
wanachama wa mfuko wa bima ya afya ni wagonjwa wanaopata huduma
bure.
alisema ni wajibu wa wa watoa huduma wa sekta ya afya kuwa wabunifu
na kuzingatia wajibu wao, maadili na kufuata masharti yaliyowekwa
na serikali ili waendelee kujijengea heshima na kulinda heshima za
sekta ya afya.
mkuu huyo wa wilaya pia alitoa weto kwa mfuko wa bima ya afya mkoani
humo kushirikiana na halmashauri za wilaya kutoa elimu kwa wadau
katika ngazi za vijijiji ili kutoa fursa kwa wadau walio vijiji kutoa
kero zao kuhusiana ubora wa huduma za mfuko .
sambamba na hilo aliwataka kuhakikisha kuendeleza kukaguzi wa vituo
vya huduma ili uweze kuangalia hali na mfuko wa afya huduma,
mazingira,ya vituo na idadi ya wafanyakazi katika vituo na hali ya
vifaa tiba na vitndea kazi pamoja kuhamasisha wananchi kujiunga na
mfuko wa afya ya jamiii.



No comments:
Post a Comment